ON POINT MEDIA

ON POINT MEDIA
Karibuni sana kwa kazi nzuri ya video za harusi mikutano na kadharika

SHIRKA LA NYUMBA LA TAIFA

SHIRKA LA NYUMBA LA TAIFA
NYUMBA YANGU MAISHA YANGU

Tuesday, 28 June 2016

RC MAKONDA ATEMBELEA BANDA LA UN KATIKA VIWANJA VYA SABASABA

Katika kuelekea kilele cha Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametembelea banda la Umoja wa Mataifa (UN) lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.

Makonda alifika katika banda hilo na kupata nafasi ya kupata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa UN kuhusu kazi ambazo zinafanywa na shirika hilo hapa nchini.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) alipotembea banda la shirika hilo lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo yanatakiwa kumfikia kila mwananchi alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa lillilopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.


Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDG's) yaliyobandikwa katika banda la UN na jinsi walivyojipanga katika kuelimisha wananchi kuhusiana na malengo hayo kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar. Kulia ni Maafisa Habari wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu na Usia Nkhoma Ledama. RC Makonda amekuwa mgeni kwanza mashuhuri kutembelea banda hilo na kutoa baraka zake kwenye maonyesho hayo.

Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu katika picha ya pamoja huku wakiwa na bango maalum linalowakilisha rangi za malengo 17 ya SDGs na mmoja wa vijana aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo kwenye ukumbi wa Karume kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kuhamasisha wananchi kutembelea banda hilo na kujifunza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu SDGs na kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo hapa nchini.

BENKI YA CRDB YAFADHILI UJENZI WA KITUO CHA MAWASILIANO CHA JESHI LA POLISI

Jiwe la Msingi la Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi lililowekwa na Rais Dk. John Magufuli. Kituo hicho kimefadhiliwa na Benki ya CRDB kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 300. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akiteta jambo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Esther Kitoka.
Brass Band ya Polisi ikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akisalimia na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (wa kili kulia) akifurahia jambo na Naibu wake (kulia), IGP,Ernest Mangu, wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisalimia na Rais John Magufuli.

Monday, 27 June 2016

Kitwanga Akabidhi Rasmi Ofisi Kwa Waziri Mwigulu Nchemba, Jijini Dar Es Salaam Leo.


SeeBait
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kushoto) pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto meza kuu) akimsikiliza aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga alipokuwa anazungumza na Waziri huyo pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano ofisini humo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa pili kulia) alipokuwa anazungumza kabla ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (wa tatu kulia) kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) mara baada ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (katikati) kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto), aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga wakifurahi jambo mara baada ya Waziri Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano katika tukio lililofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (wa pili kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. 

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA NA AFANYA MABADILIKO MADOGO YA WAKUU WA MIKOA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.

Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.

Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.

Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.

Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.

Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa).

SAFARICITY ADVERT

Matukio ya Kitchen Party ya Mary