ON POINT MEDIA

ON POINT MEDIA
Karibuni sana kwa kazi nzuri ya video za harusi mikutano na kadharika

SHIRKA LA NYUMBA LA TAIFA

SHIRKA LA NYUMBA LA TAIFA
NYUMBA YANGU MAISHA YANGU

Thursday, 18 August 2016

Wednesday, 17 August 2016

Serikali Kuchunguza Mali za Vigogo 500.........Wamo Wabunge, Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi

WAKATI takribani asilimia 20 ya viongozi wa umma kwa mwaka 2011 hadi mwaka jana hawakuwasilisha matamko ya mali zao kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa wakati, mwaka huu serikali imetangaza kuhakiki matamko ya mali za viongozi 500.

Aidha, serikali hiyo imebainisha wazi kuwa haitowafumbia macho viongozi, watakaoshindwa kuwasilisha matamko ya mali zao kwa mujibu wa sheria, ikiwemo viongozi watakaowasilisha matamko ya mali yatakayobainika kuwa na udanganyifu.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki wakati akifungua warsha ya wadau, kujadili taarifa ya matokeo ya utafiti kuhusu hali ya maadili nchini Dar es Salaam jana.

Kairuki alikiri kuwa hata katika tafiti nyingine ndogo, zilizofanyika kuhusu hali ya maadili nchini pamoja na takwimu kubadilikabadilika, lakini zilibainisha kuwepo kwa viongozi wasiowasilisha matamko yao ya mali na wengine kutowasilisha kwa wakati.

Alisema taarifa hiyo ya utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi nchini kwa miaka mitano kuanzia 2011 hadi mwaka jana, ilibainisha kuwa pamoja na kuwepo kwa mwamko wa viongozi kuhusu suala zima la maadili, bado asilimia 20 ya viongozi hao wa umma hawakuwasilisha matamko yao ya mali kwa wakati.

“Tumepokea taarifa hii na imetutia hamasa kwa kweli, tumeona asilimia 20 hawarejeshi kwa wakati matamko yao, hawa ni wengi sana ikizingatiwa kuwa ni viongozi, tunatoa onyo hakuna atakayefumbiwa macho endapo atakiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kwani atachukuliwa hatua stahiki za kisheria,” alisisitiza.

Alisema kwa kawaida endapo kiongozi asipowasilisha tamko la mali zake hadi ifikapo Desemba 31, huhojiwa na Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, lakini pia inapothibitika kuwa alikiuka kwa makusudi sheria hiyo ya maadili ya viongozi huchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema mwaka huu, kuna jumla ya viongozi wa umma 15,624 kati ya hao viongozi 500 tayari wameshatengewa fedha kwa ajili ya mali zao kuhakikiwa na endapo fedha zitapatikana idadi hiyo inaweza kuongezeka na kufikia 1,000.

“Miaka ya nyuma tulikuwa tunahakiki kwa mwaka viongozi 100 hadi 200, safari hii tumejipanga kuanza na viongozi 500. Lakini katika hili tunaomba wananchi nao watusaidie kuhakiki mali za viongozi hawa wa umma kwani sheria inawa ruhusu kufanya hivyo, ili kuweza kubaini viongozi wadanganyifu,” alisema.

Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Profesa Kessy aliyefanya utafiti huo kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi, alisema lengo la utafiti huo ni kuangalia hali halisi ya maadili nchini kuanzia viongozi hadi kwa wananchi.

Breaking News: Rais Magufuli Atengua Uteuzi Wa Mkuu Wa Mkoa Arusha Felix Ntibenda,amteua Mrisho Gambo Kuwa Mkuu Wa Mkoa

Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha,Mrisho Gambo aliyeteuliwa na Rais,kuapishwa kesho ijumaa Ikulu jijini Dar
***
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.

Tundu Lissu Atumia Dakika 120 Kupangua hoja Mahakamani ........Alikuwa akimtetea Ester Bulaya dhidi ya wafuasi wa Wasira

Tundu Lissu, ambaye ni wakili wa Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya jana alitumia muda wa saa mbili kupangua maombi ya wananchi wanne wanaopinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu yaliyompa ushindi mteja wake. 

Kesi hiyo imeanza kusikilizwa tena baada ya Mahakama ya Rufaa kufuta uamuzi wa Mahakama Kuu uliotupilia mbali hoja za kupinga matokeo hayo, ambazo ziliwasilishwa na wafuasi wanne wa aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo, Steven Wasira (CCM). 

Jaji Mohamed Gwae wa Mahakama Kuu, alitupilia mbali kesi hiyo baada ya kukubali pingamizi la Lissu kuwa wafuasi hao hawakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi hiyo. 

Wakazi hao wa Bunda wanadai kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki kutokana na kugubikwa na vitendo vya rushwa, mgombea wanayemuunga mkono kunyimwa fursa ya kuhakiki matokeo na pia kuongezeka kwa idadi ya vituo vya kupigia kura.

Jana, Lissu, ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema na wakili wa kujitegemea, alitoa majibu ya utetezi mbele ya Jaji Lameck Mlacha kuanzia saa 4.10 asubuhi na kukamilisha saa 6.02 mchana wakati shauri hilo lilipoahirishwa kwa muda hadi saa 8:00 mchana kutoa fursa kwa mawakili wa upande wa wadai, Constantine Mutalemwa kujibu. 

Lissu alidai kuwa waleta maombi wameshindwa kutoa hoja mahususi kuonyesha ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi wanazodai ulikuwepo katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana. 

Wakili Lissu pia alidai kuwa walalamikaji ambao ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malegele, pia wameshindwa kuonyesha madhara waliyopata kama wapigakura kuishawishi mahakama kutengua matokeo yaliyompa ushindi Bulaya dhidi ya mwanasiasa huyo mkongwe. 

“Waleta maombi wanadai uchaguzi haukuwa huru na haki, idadi ya wapigakura kutofautiana kwa kila kituo na uwepo wa vitendo vya rushwa, lakini hawabainishi wazi nani mhusika wa mambo wanayoyalalamikia na madhara waliyopata kwa nafasi yao ya wapigakura,” alisema wakili Lissu. 

Alisema vitendo vya rushwa katika uchaguzi ni kosa kubwa linaloweza kusababisha kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi mzima, lakini walalamikaji wana wajibu wa kumtaja mhusika wa vitendo hivyo ili kuipa mahakama fursa ya kutafsiri vyema sheria na kutoa haki. 

“Lakini madai ya juujuu tena ya jumla kuwa aliyetoa rushwa ni wakala wa mteja wangu, hayakubaliki mbele ya macho ya sheria kwa sababu mtu huyo hajulikani na jukumu la kuthibitisha madai ni la mleta maombi na uthibitisho huo haumo kwenye hati yao ya maombi,” alidai Lissu. 

Aliomba maombi hayo yafutwe kwa hoja kwamba wadai hawajataja vifungu vinavyoipa mahakama haki na mamlaka ya kuyasikiliza na kuyaamua.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KIONGOZI MKUU WA MADHEHEBU YA BOHORA DUNIANI MTUKUFU DKT. SYEDNA MUFADDAL SAIFUDDIN (TUS) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wakwanza kushoto.(Katikati ni mkalimani)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 17 Agosti, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohra Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb(TUS) Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga ambapo Rais Magufuli ameipongeza Jumuiya ya Dawoodi Bohra kwa juhudi kubwa inazofanya katika kutoa huduma za kiroho na pia kushiriki katika maendeleo.

Dkt. Magufuli amewakaribisha wana Jumuiya hiyo kuwekeza hapa nchini hususani katika sekta ya viwanda na pia amewakaribisha katika Maadhimisho ya Jumuiya ya Dawoodi Bohra duniani yanayotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam Mwezi Oktoba 2016.

"Tanzania ni nchi nzuri, tumekuwa na ushirikiano mzuri sana na wenzetu wa Jumuiya ya Bohra, hivyo njooni mfanye biashara na Tanzania,  tumepanga katika kipindi cha mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 Tanzania iwe nchi ya viwanda, kwa hiyo tunawakaribisha kuja kuanzisha viwanda vya kutosha" Amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohra Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri inayofanywa na Serikali yake ya awamu ya Tano, na pia ameahidi kuwa Jumuiya ya Dawoodi Bohra ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika maendeleo.

Aidha, Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb amemkabidhi Rais Magufuli hundi ya Dola la Marekani Elfu Hamsini na Tatu (USD-53,000) sawa na Shilingi Milioni 116 za Kitanzania kwa ajili ya kuchangia utengenezaji wa madawati ya wanafunzi kwa shule mbalimbali hapa nchini na pia amekabidhi hundi ya Dola za Marekani Elfu Ishirini na Moja (USD-21,000) sawa na Shilingi Milioni 46 kwa ajili ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amepokea barua kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Saharawi Mhe. Brahim Ghali iliyowasilishwa na Mjumbe Maalum wa Rais huyo ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Bachir Moustapha Sayed.Pamoja na kupokea barua hiyo Rais Magufuli amesema Serikali yake ya Awamu ya Tano itaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano wake na Jamhuri ya Kiarabu ya Saharawi na pia itaendelea kuunga mkono juhudi za wananchi wa Saharawi kupata haki ya kuamua hatma yao.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
17 Agosti, 2016.
 Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin akimuombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na  Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wengine katika picha ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir,  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na viongozi wengine wa BAKWATA na wa madhehebu ya Bohora.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na  Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wengine katika picha ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir pamoja na viongozi wengine wa Madhehebu ya Bohora.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuagana na  mgeni wake Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin.
PICHA NA IKULU.

Mabasi ya mikoani kugoma Jumapili

CHAMA cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) kimesema kitasitisha huduma ya kusafirisha abiria kwenda mikoa yote nchini Jumapili ili kufanya ukaguzi wa mabasi yake, hatua ambayo itakuwa sawa na mgomo.

Aidha, Taboa imesema inapinga uamuzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) kutangaza kuyafungia mabasi yote ya kampuni ya City Boy badala ya moja ambalo lilisababisha ajali mkoani Singida hivi karibuni.

Julai 4, mabasi mawili ya kampuni hiyo yaligongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30 wilayani Manyoni mkoani Singida.

Taboa imesema pia itaipeleka serikali mahakamani kutokana na kufungiwa kwa mabasi hayo kwani kwa mujibu wa sheria, aliyetakiwa kulifungia ni waziri mwenye dhamana na si Sumatra kama ilivyofanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kumaliza kikao cha dharura cha wamiliki wa mabasi ya mikoani, Katibu wa Taboa, Enea Mrutu, alisema hawatakatisha tiketi kuanzia Jumapili ili kujipa muda wa kukagua mabasi yao kama yana uwezo wa kufanya safari ama la.

"Tumeamua kwa pamoja kuwa, kwa sababu tayari tumeshafanya 'booking' ya abiria, kuanzia Agosti 21 mwaka huu, tuanze kufanya ukaguzi wa mabasi yetu kote nchini ili yale ambayo hayana sifa yakae pembeni na yale yanayostahili kusafirisha abiria yafanye hivyo, kuliko utaratibu huu wa serikali wa kuyafungia yote bila kujali gari lililohusika kwenye ajali," alisema Mrutu.

Aidha alisema wanapinga vikali agizo la Sumatra la kuyafungia mabasi 60 ya kampuni 12 kwa makosa ya kusababisha ajali na wanataka mabasi yanayohusika pekee ndio yafungiwe.

Alizitaja kampuni zilizofungiwa mabasi yake kuwa ni Mohamed Trans, City Boy, Ota High Class, Kisbo Safari, Kisbo Express, Lubonelo na Kanda Safari.

Mrutu pia alisema kikao kicho kilipinga azimio la serikali kutaka mabasi yanayoenda masafa marefu kama mikoa ya Mwanza na Mbeya kutumia siku mbili na badala yake yatumie siku moja kama ilivyokuwa awali.

Alitaja azimio la tatu kuwa ni kufunga mfumo maalum wa udhibiti wa magari (Car Track System) ambao utaunganishwa na ule wa Sumatra ili kuliona gari lilipo kwa lengo la kudhibiti ajali.

Aidha, Mrutu alisema wamekubaliana mabasi yote yatatembea kilometa 80 kwa saa moja na 50 pale inapohitajika kama kwenye matuta ili kuepuka ajali.

Alisema wamekubaliana pia dereva atakayehusika kutembea zaidi ya mwendo waliokubaliana, afukuzwe kazi na kumchukulia hatua stahiki.

"Kama magari yetu tutayafanyia ukaguzi na pia kufunga kifaa cha kulionyesha basi na kupunguza mwendo, hakuna haja tena ya kutaka tusafiri zaidi ya siku moja... maeneo wanayoona kuna hatari ya usalama ni bora yakasubiriana na askari wakayasindikiza mpaka yanapokwenda," alisema.

Aliendelea kueleza kuwa wamekubaliana Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, awahakikishie hakuna askari atakayedai mabasi hayo rushwa.

Mrutu alisema wamekubaliana mabasi yasikaguliwe kila kituo ili kuepuka kupoteza muda wakati wakisafiri kwenda mikoani ambako kunasababisha madereva kutembea mwendo kasi ili kuokoa muda waliopoteza njiani.

Tuesday, 16 August 2016

Rais Dkt. Magufuli Amjulia Hali Spika Wa Bunge Job Ndugai Pamoja Na Waziri Mkuu Mstaafu John Samuel Malecela Jijini Dar Es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana kwa furaha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Sala sala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai nyumbani kwake Sala sala jijini Dar es Salaam alipokwenda kumjulia hali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli kushoto akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai nyumbani kwake Sala sala jijini Dar es Salaam walipokwenda kumjulia hali. Kulia ni mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Spika Sala sala jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela ambaye anapata matibabu jijini Dar es Salaam. 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimsalimia Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela ambaye anapata matibabu jijini Dar es Salaam. 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Sala ya kumuombea Waziri Mkuu mstaafu John Samwel Malecela pamoja na mkewe Anne Kilango Malecela. 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na Mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai wakati alipokwenda na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai huku Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WASTAAFU WA NHC WAAGWA KATIKA TAFRIJA MCHAPALO ILIYOFANYIKA MAKAO MAKUU YA NHC

Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgdg-DWweO-dEFOGiYLMkBzuDPikyxHekxymQglWCkLuH32L6dszFUGrHGaEr0je7gYZbF4rljO98XPYYNZaEYrK3Gr8GAQsacqJ2NXDpJKjUa5fcGBxZD2MXT2LN-13daoTPX0aYTZcLeO/s640/_DSC0505.JPG
Wastaafu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mama Clara Ngalioma na Mama Habiba Kitalima waliotumikia Shirika la Nyumba kwa uadilifu mkubwa kwa kipindi cha takribani miongo mitatu na kustaafu rasmi Juni na Julai mwaka huu. Hafla fupi ya kuwaaga wastaafu hao ilifanyika Ijumaa jioni Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE.

Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEha80oqkEUrW6cLHT6qe0uCMAtgM3gRUuHtKMyqKRtgCwnVTN9V8Zd9DtO_zB4I44uC4V-rrUkxJGHBrCJ4AZiKCTGhpmC_LfSM__kFR47QWHtgdsGeZ5nGrWR4xiq0l-j_6UOo4toB_uYo/s640/_DSC0480.JPG
Wastaafu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mama Clara Ngalioma na Mama Habiba Kitalima waliotumikia Shirika la Nyumba kwa uadilifu mkubwa kwa kipindi cha takribani miongo mitatu na kustaafu rasmi Juni na Julai mwaka huu. Anayeshereheka nao ni Rudya Taraba wa Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC. Hafla fupi ya kuwaaga wastaafu hao ilifanyika Ijumaa jioni Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE.
Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiO7245qtBcjRWe_41z0SYvaGbF7gP7eg7XahHXHNEsybBgxcgsNm7Mu6Oew2jVlpa8crXt_Oh5x2NFCj55WfTt1ZKCa3GuJvXs5d0xnm4jhrCKBPRfLTnpK6JBFPMoOK1LibmxZfdW6vBQ/s640/_DSC0412.JPG
Ofisa Utawala wa NHC, Veronica Mtemi na Rudya Taraba wa Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC wakishereheka pamoja katika hafla ya kuwaaga Wastaafu Mama Clara na Mama Kitalima. Hafla fupi ya kuwaaga wastaafu hao ilifanyika Ijumaa jioni Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE.
Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0yXdQWpBbQiordHXQ38LQBEM1RAzgTSiZ-3b73E9VimgIjkR-B3JR9dASASDfCJoJImNvLWYHd5drcqUf2HMu3-5eFdtuVHQa3718l4gn_lUyTmxkc-1cCtYCQgW4HPfHpMDuUfB7_sCT/s640/_DSC0415.JPG
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio akibadilishana mawazo na Mstaafu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mama Clara Ngalioma.
Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhGJiNzEIVSRaR8JjzVpb3Yc5uoWy_B4FdR3IcqWXUi1E6HTFf-9BhyphenhyphenkSQx6OHFgcwUb4Uk_4GgsSY8kYRqeHa3GdwZ516Jwiv9gRtcamIBO3eDGekFqOTpzL2i6CFilCGk_dXaZHdb-8UQ/s640/_DSC0416.JPG
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa, Susan Omari  akisalimiana na Mama Habiba Kitalima katika Tafrija Mcapalo iliyofanyika Makao Makuu ya NHC.
Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgGVomPi-M0adh2akQhXgxe5R0yffWBmc4f5AhRfL4O3eKeY4o-9Ij92wA8bvLSvymoBt6iqWDHvVDVN1Z1Ir32zWnHMV2ZxheoABDOmL7ZN6HJ8rUxNafJKSWqWHu_cVGq2MIkEEwz-rBh/s640/_DSC0419.JPG
 Godlove Godwin na Humprey Tarimo mawazo wakati wa tafrija mchapalo hiyo iliyofanyika Ijumaa Jioni.
Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEibepc1WTYJaRTLaDiCG0bzVyugoyN7MhgBvgrSiHRbZmC1jJ3zEQlyASvJ_TwsUhkfYKguiIAc7d3izocIfdmBu1NwkqsapUlS3i0G0SehzuTtsEcTClT-bKasn8Pzw4HDoiF7n0gRTZPS/s640/_DSC0421.JPG
 Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Pius Tibazarwa akisalimiana na Mama Habiba Kitalima katika Tafrija Mchapalo iliyofanyika Makao Makuu ya NHC.
Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjiWKknEth_0m5CaGewPt_VYDcn3_QTpYYE8WyjCd_SuIeX3GSGywkzrFkp_ph89GKcA6npRdFNCRvZXX9LZcin6CLXcgd4Ql8eNKVcsfe0StbyS33DbRev5KW3KqVIVGBMesPz-9JUzAgf/s640/_DSC0435.JPG
  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Pius Tibazarwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji Mikoa na Utawala wa Shirika la Nyumba la Taifa, Raymond Mdolwa wakibadilishana mawazo katika Tafrija Mchapalo iliyofanyika Makao Makuu ya NHC.
Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiw_P0MqwJCsHYk21PVnQma2XlnAl4vQvSMtUUejK1rjYJ16JibLPVJkIMCR0CpQVcJCEK3iAftYniKNhiG-bBG3P3BqXEqXWWQfGUQ-ZAeojykTWFS_mrbv1__mQf7meAb9191kgHASggG/s640/_DSC0464.JPG
 Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu wa Shirika la Nyumba la Taifa, James Rhombo akibadilishana mawazo na wafanyakazi wa NHC katika Tafrija Mchapalo iliyofanyika Makao Makuu ya NHC.
Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhzJTNHPN1mRs-TKyCFM35wdVdeVjqzFt_MzmHpD0xCjpQkvg1lclsDraijVnlfzu2FxBZ0dy9ZFGk8EGs-D-EyxHA1vkm43jQ16sZ0KpPDqFeK3pTFbs_-yR1d64QnGZtq9ieRGUs1Nzrm/s640/_DSC0477.JPG
 Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (TAMICO) Iddi Kitete akibadilishana mawazo na wafanyakazi wa NHC katika Tafrija Mchapalo iliyofanyika Makao Makuu ya NHC.

Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgCUvsAJZpIE4E7cZTrPiAXaqeTzuKu9Spw_J9RBsTySg75EASJqc8lZ0nUj9PlD3sPLgh-98DJjiGX8vdthqvhSRLeqLLU-OQ3eZK9GoZpp2EXJ74Yn2VmETI8nx_pfTUsyuqmTeM0m4A3/s640/_DSC0481.JPG

Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjG-BuRGdDbq72sz1jOVKiAtulupLOKWAeWC69DRVWQdMns5ij0CLN40zPaUIGevWEtj1sRf9ncvcvmft5bvz53voV9r757D-gcG19f123z9sRgPYq6PTaFbUZsNVz7oAsmArixmhXxh8gp/s640/_DSC0488.JPG

 Sixtus Killenga na William Bukuru wa NHC wakiendelea kushereheka katika tafrija mchapalo hiyo.
Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGoHtcWmrA0tAnR2vV3LrI1vQoC7OucBS_NDzupWnogQuskGc2lHBajv7w9sDJlL7NWFBq4dvck85FwFczspp23uwRBBTRrluK2sdCd-SPxc69dknmDn9M2TAYI4r4oQ_blUbMrP_SdWew/s640/_DSC0511.JPG
 Wastaafu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mama Clara Ngalioma na Mama Habiba Kitalima wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa.
Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgtGxOh1qhWrTf93Qx32DTB0QLoFuColJZzsilMz4zWoh3nkcoGcX99nZxAmgB8wdPJjZeZT8926Rg1H7J4F3MIpwahbT-XpmvpPccyze5lCqPalftDBSAXIcANzfvTIQwa1Xhu2uHAYKly/s640/_DSC0513.JPG
  Wastaafu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mama Clara Ngalioma na Mama Habiba Kitalima wakiwa katika picha ya pamoja na waliokuwa wafanyakazi wenzao.
Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjA2YtYbIVxR_75qcmIA5F0iAZWoTWYgXgEFemgiOSlL_3PVCab6yZ2AYJFzuJdv_qcOufVRyZxalrFFBjkMcCEjPqca-w1GmKVkLvBlkwHfb9xlsRId4YRgdTUzNKuUb22QiKJmWSDHyIy/s640/_DSC0515.JPG