ON POINT MEDIA

ON POINT MEDIA
Karibuni sana kwa kazi nzuri ya video za harusi mikutano na kadharika

SHIRKA LA NYUMBA LA TAIFA

SHIRKA LA NYUMBA LA TAIFA
NYUMBA YANGU MAISHA YANGU

Friday, 23 September 2016

Kikwete Atunukiwa Tuzo Ya Uongozi Wa Kisiasa Na Utetezi Seebait.com 2016



 Na  Mwandishi Maalum, New York

Shirika lisilo la  Kiserikali    la Speak  Up for Afrika    limemtunukia tuzo, Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kutokana na uongozi wake wa kisiasa na utetezi wake  kwa  makundi ya jamii yaliyo katika mazingira magumu hususani wanawake na watoto.
  
Utoaji wa  Tuzo hiyo  ya  uongozi wa kisiasa na utetezi , umekwenda sambamba na   hafla ya  miaka mitano ya kuanzishwa kwa  Taasisi ya Speak up  Afrika. Hafla  hiyo iliyofanyika jana Alhamisi Jijini New York   ilikuwa  pia  ni sehemu ya kuhamasisha uchangiaji   wa shughuli za  Taasisi hiyo.
  
Mchango ambao umetambuliwa na  Speak Up  Afrika,   taasisi ambayo imekuwa ikifanya kazi  kwa Karibu na Rais Mstaafu Kikwete, ni  katika maeneo ya  upelekaji na usambazaji wa huduma za msingi za afya hususani afya ya mama na mtoto,  udhibiti wa  ugonjwa  wa malaria kupitia kampeni  ya malaria haikubaliki ,usambazaji wa vyandarua  vyenye viatilifu, kampeni ya  lishe bora, na  kampeni ya   chanjo kwa watoto.
  
Pamoja  na  kutambua  juhudi za   Rais Mstaafu  Kikwete katika  kuyasemea maeneo hayo,  Taasisi hiyo kupitia  Mkurugenzi wake  Mtendaji Bi. Kate Campana pia imemtambua  kama kiongozi ambaye    amekuwa mstari wa mbele  wa kulisema Bara la Afrika kila  mara alipopata  fursa  ya  kufanya hivyo wakati akiwa madarakani na hata baada ya kustaafu.
  
Rais kikwete ameelezwa katika hafla hiyo iliyowashirikisha  wadau wa kada mbalimbali, kama kiongozi wa kisiasa ambaye amezigusa nyoyo za watu wengi kujitolea kwaajili ya watu wenye mahitajio ya kupata huduma za msingi za kijamii ambazo  au wameshindwa kuzipata kutokana na kipato kidogo au haziwafikii kabisa.
  
Akipokea  Tuzo hiyo, Rais  Mstaafu Kikwete , amesema Tuzo hiyo ni ya watoto wote  waafrika ambao ndio  waliomfanya asimame   mbele ya wageni waalikwa.
  
“ Ni kwa sababu yenu ndio sababu nimetenga muda wangu  baada ya kustaafu kusukuma mbele agenda ya  kuboresha maisha yanu. Ninafanya hivyo kwasababu makuzi yangu yalikuwa kama  ya mtoto yeyote yule wa  kiafrika, nimeyaishi maisha  wanayo ishi. Na kwa hiyo ninaelewa fika  hamu na kiu yao ya kuwa  na maisha bora na afya njema”. Akasema Kikwete na kushangiliwa na wageni waalikwa.
  
Akaongeza kuwa  ,  mafaniko ambayo ameyapata katika  juhudi hizo  za kufikisha huduma za msingi  za kijamii kwa makundi  yenye mahitaji  yametokana na mambo mawili makubwa moja ni   aina ya uongozi  alioutumia kusukuma harakati hizo. Na pili  uhamasishaji uliofanyika katika  kupiga vita malaria kupitia Speak Up Afrika na    kampeni yao ya  malaria haikubaliki.
  
“ Nisingeweza kuyafanya niliyoyafanya   bila uungugwaji mkono na  ushirikiano  wa karibu nilioupata  na ninaoupata kutoka taasisi za kimataifa  ikiwamo hii ya  Speak Up  Afrika. Ndio maana  kwa mfano,  tumeweza kupunguza visa vya malaria kwa   theluthi mbilli,  tumefanikisha  upatikanaji wa chanjo kwa asilimia 96 kwa watoto wote na kupunguza vifo vitokanavyo na  malaria kwa   nusu.” Akaeleza Kikwete na kushangiliwa  tena.
  
Akasema, anamini katika ushirikiano na wadau mbalimbali  kama akina Ray Chambers kupitia kampeni ya  hakuna tena malaria, Taasisi ya  Bili na Melinda Gates na Gavi Vaccination   Alliance ambayo anashirikiano  nayo kwa karibu katika  kampeni ya chanjo kwa wote.
  
Rais  Mstaafu amewahakikishia   watendaji wa Speak  Up Afrika kwamba  ataendelea kufanya kazi nao kwa karibu  kutokana  kile alichosema amejionea mwenye kazi nzuri wanayoifana.
  
 Akawasihi  wadau mbalimbali  kuichangia taasisi hiyo  kwa kile alichosema, inafanya kazi kubwa  ya siyo tu kufikisha huduma za kijamii pale zinapotakiwa lakini  pia imekuwa ni kipaza sauti cha Afrika.
  
Wengine waliopewa Tuzo kwa kutambua michango yao kwa jamii ni  pamoja na   Professa Awa Marie Coll- Seck, Waziri wa Afya  wa Senegal, Bibi Toyin  Saraki,  mwanzilishi wa Taasisi ya  Wellbeing  Afrika ambayo  pia imekuwa ikitoa  elimu na misaada kwa wanawake na watoto pamoja na elimu  kwa wakunga na kutambua kazi nzuri, kubwa na ngumu  ya kuwahudumia wanawake wenzao wanapojifungua.  Na  Bwana Kabirou Mbodje ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa  Taasisi ya  Wari.
  
Taasisi ya  Speak  Up  Afrika  imeanzishwa  na wanawake na inaongozwa na wanawake. Ni taasisi ambayo imejijengea uweo na sifa kubwa ndani  ya kipindi cha miaka mitano tangu  kuanzishwa kwake

Thursday, 15 September 2016

Mabaki yaliyopatikana Pemba, Tanzania ni ya MH370


Mabaki ya ndege yaliyopatikana Pemba
Image copyrightSERIKALI, TANZANIA
Mabaki ya ndege yaliyopatikana katika pwani ya visiwa vya Pemba nchini Tanzania yalitoka kwa ndege ya shirika la Malysia Airlines iliyotoweka mwaka 2014, maafisa wa Malaysia wamethibitisha.
Waziri wa uchukuzi wa Malaysia Liow Tiong Lai amesema kupitia taarifa, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kwamba baada ya uchunguzi imebainika kwamba kipande hicho kikubwa cha bati kilichopatikana mwezi Juni ni cha ndege hiyo safari nambari MH370.
Amesema uamuzi huo ulifikiwa na wataalamu kutoka Idara ya Usalama wa Safari za Ndege ya Australia (ATSB) na wale wa kuchunguza usalama wa MH370.
Mapema Julai, waziri wa uchukuzi wa Australia Darren Chester alikuwa amedokeza kwamba kulikuwa na uwezekano mkubwa mabaki hayo yalikuwa ya ndege hiyo.
Alisema muundo wa mabaki hayo, ukubwa wake na muonekano wake viliashiria kwamba yalikuwa ya ndege hiyo ya Malaysia.
Mabaki hayo pia yalikuwa na muhuri wa kuonesha tarehe ya kuundwa kwake ambayo ilikuwa Januari 23, 2002. Ndege hiyo ya Malaysia iliwasilishwa kwa shirika hilo 31 Mei, 2002, kwa mujibu wa tovuti ya shirika la Channel News Asia.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilitoweka Machi 2014, ikiwa na abiria 239 baada ya kupaa kutoka Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia kuelekea Beijing.
Bw Liow amesema mabaki hayo yatachunguzwa zaidi kubaini iwapo kutapatikana ufumbuzi kuhusu kilichotokea hadi ndege hiyo ikatoweka.
Awali, wachunguzi walikuwa wamethibitisha kwamba mabaki yaliyopatikana visiwa vya Reunion mwezi Julai 2015 yalitoka kwa ndege hiyo.
Mabaki mengine yanayodhaniwa kutoka kwa ndege hiyo yamepatikana Msumbiji, Afrika Kusini na visiwa vya Rodrigues, Mauritius.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Septemba 14

PICHA: MAKAMU WA RAIS ALIPOMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA RAIS WA AWAMU YA 6 WA ZAMBIA

lungu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu  Septemba 13, 2016.
 Rais Robert Mugabe akisalimiana na Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt Kenneth Kaunda
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Botswana Luteni Jenerali Seretse Khama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe william Rutto,  Makamu wa Rais wa Namibia Mhe. Nickey Iyambo na Rais wa kwanza wa Zambia Dkt. Kenneth Kaunda baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu Septemba 13, 2016
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe william Ruttona wageni wengine wakielekea jukwaani  kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka ambako amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu Septemba 13, 2016.
 Rais mteule wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu akila kiapo kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kwenye sherehe za kuapishwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia  Septemba 13, 2016
Rais Robert Mugabe wa Zambia akizungumza kwa niaba ya viongozi waalikwa wote
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akimpongeza Makamu wa Rais  wa Zambia Mama Inonge Mutukwa Wina kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu Septemba 13, 2016
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akinong’onezwa jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya watoto Mhe. Agnes Musunga baada ya sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu  Septemba 13, 2016

JK Atoa Ya Moyoni Kuhusu Rais Magufuli Kutokwenda Zambia

Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ameunga mkono uamuzi wa Rais John Magufuli kuahirisha safari kwenda nje ya nchi ili kushiriki katika maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.

Kikwete amesema uamuzi huo ni wa busara kwa kuwa Serikali inatakiwa kufanya juhudi za makusudi kushughulikia tatizo hilo.

Kikwete aliyemtumia salamu za pole Dk Magufuli na waathirika wa tukio hilo, amesema misaada ya haraka na dharura inahitajika ili waathirika waendelee kupata huduma zote muhimu hasa za kibinadamu.

Kiongozi huyo mstaafu ameyasema hayo  katika hafla ya makabidhiano ya nyumba 22 za watumishi wa afya, 10 zikiwa Chalinze, mbili Bagamoyo na nyingine 10 Mafia zilizojengwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa mkoani Pwani.

“Ndugu zangu pamoja na leo hii tunakabidhiana nyumba 22 za watumishi wa afya mkoani kwetu, naomba tusimame tuwakumbuke wenzetu waliopoteza maisha katika tetemeko la ardhi huko Bukoba na pia natumia fursa hii kutoa pole kwa waathirika wote na Rais Dk Magufuli,” amesema.

Ameongeza kuwa: “kiukweli amefanya uamuzi wa busara kuahirisha safari yake ili kushiriki katika maafa haya.”

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika Kituo cha Afya Msoga, Chalinze.

TAARIFA KUHUSU MADEREVA WA TANZANIA KUTEKWA NA WAASI WA MAI MAI

whatsapp-image-2016-09-15-at-8-34-33-amChama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo nchini Tanzania (TATOA) kinaripoti kwamba, waasi wa Mai Mai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamewateka nyara madereva wa Tanzania na kuchoma baadhi ya magari ya mizigo. Waasi hao wanadai dola za Kimarekani elfu nne (karibu shilingi za Kitanzania milioni tisa) kwa kila dereva ama sivyo watawapiga risasi madereva wote. Pia waasi hao wametoa siku ya mwisho (deadline) ya majeshi yanayolinda amani nchini humo kuondoka.

TATOA inasema imezungumza na mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics, Mzee Azim Dewji ambaye amethibitisha taarifa hizi na pia balozi wa Tanzania DRC pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje tayari serikali inashughulikia suala hili. Jumla ya magariyaliyotekwa ni 12 kati ya hayo magari 8 ya Tanzania na 4 ya Kenya. Magari 4 ya Tanzania yamechomwa moto na madereva wote walichukuliwa na waasi lakini bahati nzuri madereva wawili wa Tanzania walifanikiwa kuwatoroka. Tukio hilo limetokea sehemu inaitwa Kasebebena na Matete, wastani wa kilomita 30 kutoka mji wa Namoya.
TATOA inawashauri wanachama waliopakia mzigo kuelekea huko kuwasiliana na madereva wao ili wasitishe safari, kusubiri taarifa ya hali ya usalama kutolewa.
Mai Mai Kata ni kundi la waasi nchini DRC ambalo linadai kupigania uhuru wa jimbo la Katanga, na linaongozwa na Gédéon Kyungu Mutanga, ambaye aliunda kundi hilo mara tu alipotoroka kutoka gerezani mwaka 2011.