ON POINT MEDIA

ON POINT MEDIA
Karibuni sana kwa kazi nzuri ya video za harusi mikutano na kadharika

SHIRKA LA NYUMBA LA TAIFA

SHIRKA LA NYUMBA LA TAIFA
NYUMBA YANGU MAISHA YANGU

Wednesday, 3 June 2020

TAASISI YA MIKOPO YA NYUMBA (TMRC) YATOA MCHANGO WAKE KWA SERIKALI

    

TMRC imetoa msaada huo kwa hospitali ya rufaa ya mkoa ya Amana.  Msaada huo ni gallons 50 za lita 5 za vitakasa mikono (sanitizer) ambazo kwa ujumla wake ni lita 250.

Msaada huo ulipokelewa na Mganga Mkuu wa hospitali hiyo ya Amana Dr. Amani Malima, ambaye wakati wa kupokea msaada huo ameishukuru serikali kwa ushirikano wanaopata kutokana na hospitali hiyo kuteuliwa kuhudumia wangonjwa wa CORONA, Pia Dr. Amani ameishukuru Taasisi ya mikopo ya nyumba Tanzania (TMRC)  kwa mchango walioutoa wa lita 50  za vitakasa mikono (sanitizer) amesema mchango huo utawasaidia sana hasa watoa huduma wa hospitalini katika kujilinda na maambukizi ya CORONA, pia ametoa wito kwa taasisi zingine kuiga mfano uliotolewa na TMRC katika kuhakikisha tunalimaliza janga hili la ungonjwa wa  Corona, amesema mpaka sasa wamebakiwa na mgonjwa mmoja tu mwenye maambukizi ya virusi vya  CORONA Pia ametoa wito kwa jamii kuendelea kuchukua tahadhari ili kujikinga na  maambukizi ya ugonjwa wa  corona na kuhakikisha janga hili tunalimaliza kabisa.


Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC Oscar Mgaya alisema kuwa msaada huu ni mchango wa taasisi hiyo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona.  Ndugu Mgaya aliisifu sana hospitali ya Amana kwa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo. “Sisi kama taasisi tuliona ni muhimu tutoe mchango huu mdogo kwa hospitali ya Amana kama namna ya kuwasaidia na mapambano dhidi ya ugonjwa huo”

























Monday, 18 March 2019

HALMASHAURI ZATAKIWA KUINGIA MKATABA NA NHC KUJENGA NYUMBA

HALMASHAURI ZATAKIWA KUINGIA MKATABA NA NHC KUJENGA NYUMBA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi amezitaka halmashauri nchini kuingia mkataba na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba na Ofisi kutokana na  Shirika hilo kuwa na uzoefu wa kujenga nyumba zenye ubora na gharama nafuu.

Lukuvi aliyasema hayo tarehe 18 Machi 2019 wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili na Utalii ilipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba 20 katika eneo la chatur Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Kati ya nyumba hizo, kumi ni za Halmashauri ya Wilaya ya Muheza na nyumba nyingine kumi ni za Shirika la Nyumba.

Alisema, wakati wa kuingia mkataba  wa ujenzi wa Nyumba au Ofisi Halmashauri hizo zinapaswa  kuwa na fedha pamoja na kuandaa miundo mbinu (Maji, Umeme n.k) ili kuepuka kuchelewa kukamilisha ujenzi. 


Mh. Lukuvi amelipongeza Shirika kwa kuendelea na ujenzi wa nyumba hizo licha ya Halmashauri kuchelewesha malipo kwa ajili ya ujenzi huo..

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiongozwa na Kaimu Mwenyeketi wake Shaban Shekilindi walihoji kuchelewa kwa mradi wa ujenzi wa nyumba hizo za Halmashauri lakini walielezwa hali hiyo imesababishwa na Halmashauri kuchelewesha malipo ya  fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Nassib Mmbaga aliwaambia wajumbe wa Kamati kuwa Halmashauri yake ilichelewa kutoa fedha za ujenzi kwa wakati kutokana na kutumia fedha kujenga madarasa kufuatia kuwepo idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za msingi ambao wana uhaba wa madarasa. Hata hivyo, Mkurugenzi huyo Mtendaji alieleza kuwa tatizo hilo lishatatuliwa na kuahidi kulipa kiasi cha  fedha kilichobakia kulingana na mkataba.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alilitaka Shirika la Nyumba la Taifa kufanya kazi kibiashara na kuacha tabia ya kufanya kazi kwa ushawishi wa mtu au kisiasa kwasasbu kwa kufanya hivyo kutapelekea kutouzika kwanyumba zinazojengwa hivyo Shirika litaingia kwenye hasara.
 

Mradi wa nyumba 20 uliopo eneo la chatur katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga.

  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi (Aliyesimama) akisoma taarifa ya Wizara kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Dkt. Maulidi Banyani alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa nyumba za makazi chatur

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika, Dkt. Maulidi Banyani alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa nyumba 20 za makazi unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa 



 Kaimu Mwenyeketi wa  kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii  Shaban Shekilindi mwenye shati jeupe ( wa pili kutoka kulia)  akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya shirika la nyumba la Taifa Dkt. Sophia Kongela (wa kwanza kutoka kulia), Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulidi Banyani (wa pili kutoka kushoto) pamoja na Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa ndani wa Shirika Bw. Abdallah Migila (wa kwanza kushoto).
  Mhe. Lukuvi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (wa pili kutoka kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Agelina Mabula ( mwenye reflector ya njano) wakiwa na wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea mradi wa makazi uliopo katika eneo la chatur 
 wilaya ya Muhuza



  Mhandisi Mannig Mwalwaka ambaye ndie msimamizi wa mradi huo akitoa maelezo ya mradi huo

Thursday, 24 January 2019

NAIBU WAZIRI DK MABULA ARIDHISHWA NA UJENZI WA NHC KATIKA MJI WA SERIKALI MTUMBA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa ofisi za wizara katika mji wa serikali ya Mtumba mkoani Dodoma unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Dk Mabula alitoa kauli hiyo leo tarehe 22 Januari 2019 wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa ofisi za Serikali katika mji wa Mtumba mkoani Dodoma unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo liko chini ya Wizara yake.
Alisema kazi inayofanywa na shirika la Nyumba la Taifa kujenga ofisi za Serikali katika mji huo kwa sasa unaenda kwa kasi na unatia moyo jambo linalooonesha kuwa mradi wa ujenzi wa ofisi hizo utakamilika katika muda uliopangwa.
Katika mradi huo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia kampuni yake ya ujenzi inajenga ofisi za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Fedha na Uchumi, Wizara ya Nishati pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara.
Aidha, Dk Mabula amefurahishwa na ufuatialiaji wa ujenzi wa ofisi hizo unaofanywa na Wizara ya Fedha pamoja na Viwanda na Biashara na kueleza kuwa hatua hiyo inalifanya Shirika hilo kufanya kazi kulingana na mahitaji ya wateja wake.
Alibainisha kuwa, pamoja na changamoto ya kukatika umeme lakini NHC imejitahidi na kilichomfurahisha ni kuwepo vifaa vyote vya ujenzi kwenye eneo la ujenzi jambo linalompa faraja kuwa hakuna kitakachokwamisha ujenzi kukamilika kwa wakati
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amepongeza jitihada znazofanywa na Rais John Pombe Magufuli za kuhamishia Makao Makuu ya Serikali Dodoma na kubainisha kuwa hatua hiyo inatimiza ndoto ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Emma Lyimo alilisifu Shirika la Nyumba la Taifa kwa kasi kubwa wanayoendelea nayo kwenye ujenzi wa ofisi ya Wizara yake na kubainisha kuwa pamoja na kuchelewa kuanza ujenzi lakini kasi wanayoenda nayo ana imani ujenzi utakamilika kwa wakati.
Naye Msimamizi wa ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo la Makazi Mhandisi Grace Musita alisema, ujenzi wa ofisi umefikia asilimia sabini na tano na anatarajia utakamilika katika tarehe iliyopangwa kwa kuwa wamefikia hatua nzuri ya kukamika.

 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akiangalia maendeleo ya Ujenzi ya Ofisi ya Wizara ya Nishati katika mji wa Serikali wa Mtumba, kushoto ni Mhandisi wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Elisante Ulomi na katikati ni Mkurugenzi wa uendelezaji miliki Shirika la Nyumba la Taifa Haikameni Mlekio.


  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akioneshwa moja ya kifaa kitakachotumika katika Ujenzi ya Ofisi ya Wizara ya Nishati katika mji wa Serikali wa Mtumba mkoani Dodoma, kulia ni Mhandisi wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Elisante Ulomi na kushoto ni Mkurugenzi wa uendelezaji milikShirika la Nyumba la Taifa Haikameni Mlekio.


 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akimsikiliza Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Viwanda na Bisahara Emma Lyimo (Kulia) wakati alipotembelea maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya Wizara ya Viwanda na Biashara katika mji wa Serikali wa Mtumba mkoani Dodoma, kushoto ni Mhandisi wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Hassan Mohamed.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akiongozwa na Mhandisi wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Grace Musita kukagua ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika mji wa Serikali eneo la Mtumba Dodoma .


 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula katikati akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika mji wa Serikali wa Mtumba kutoka kwa Mkurugenzi wa uendelezaji milikShirika la Nyumba la Taifa Haikameni Mlekio wakati alipofanya ziara, kushoto ni Mhandisi wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Grace Musita.






Monday, 3 December 2018

MKURUGENZI MKUU NHC AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA MOROGORO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dkt. Maulidi Banyani alifanya ziara ya siku mbili katika mkoa wa Morogoro na kutembelea miradi mbalimbali akianzia katika Halmashauri ya wilaya ya Malinyi ambapo Shirika la nyumba la Taifa linajenga jengo la Halmashauri  ya wilaya ya Malinyi kama Mkandarasi,
Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulidi Banyani ameagiza ifikapo  tarehe 29/05/2019 jengo liwe limekamilika na kukabidhiwa kwa Halmashauri.

Baada ya kutoka katika Halmashauri ya wilaya ya Malinyi ziara hiyo ilielekea katika wilaya ya Mvomero ambapo shirika limejenga nyumba  42. 

Vilevile Mkurugenzi Mkuu Dkt. Banyani alitembelea Jengo la biashara na ofisi la 2D lililopo Morogoro Mjini, Dkt. Banyani alitoa agizo kwa Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa, Verenanda Seif kuhakikisha wanalitangaza jengo hilo ili lipate wapangaji wa kutosha tofauti na sasa ambapo asilimia 30 tu ndio iliyochukuliwa sehemu kubwa ikiwa ni mabenki
pia akatoa agizo kwa mameneja wote pindi wanapopangisha jengo wawe wanapiga picha jengo kabla ya mpangaji kuingia ili anapoondoka akabidhi likiwa bora kama alivyokabidhiwa na si vinginevyo.
Pia alitembelea Plot No 31- 34 Nkomo, Plot No 66/2 OLD DSM ROAD, PLOT 53 KINGO  mwisho alimaza ziara kwa kutembelea Shule ya Sekondari Mzumbe iliyokarabatiwa na Shirika. Mkuu wa Shule alilipongeza Shirika kwa kufanya kazi nzuri na yenye weledi na kutoa wito kwa Serikali kwa miradi kama hiyo wapewe NHC kwani wamefanyakazi nzuri sana na kwa wakati.

Jengo la Halmashauri  ya wilaya ya Malinyi linavyoonekana kwa sasa
Dkt. Maulidi Banyani akiwa ameongozana na Kaimu Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa ndani Abdallah Migila pamoja Meneja wa mkoa wa Morogoro Veneranda Seif wakiwa katika mradi wa jengo la Halmashauri  ya wilaya ya Malinyi.


Mhandisi Hassan Mohamed akitoa maelezo ya mradi kwa Mkurungezi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani 



Mhandisi Hassan Mohamed akitoa maelezo ya mradi kwa Mkurungezi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani



Mkurungezi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani akitoa maelekezo wakati alipotembelea mradi huo wa jengo la Halmashauri  ya wilaya ya Malinyi unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa.
Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulidi Banyani akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri  ya wilaya ya Malinyi Mussa Mnyeti  alipotembelea katika mradi wa jengo Halmashauri  ya wilaya ya Malinyi linalojengwa na NHC 


Picha ya pamoja kati ya watumishi wa  Halmashauri  ya wilaya ya Malinyi na Shirika la Nyumba la Taifa.


Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulidi Banyani akiwa  na Kaimu Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa ndani Abdallah Migila, Baraka Killungu  wakiwa na  Meneja wa mkoa wa Morogoro Veneranda Seif wakiwa katika  Nyumba za makazi Mvomero.

Nyumba za makazi 42 zilizojengwa  katika Halmashauri ya wilaya ya Mvomero
Mkurugenzi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani wakijadiliana jambo  na Kaimu Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa ndani Abdallah Migila walipotembelea Nyumba za makazi 42 zilizojengwa  katika Halmashauri ya wilaya ya Mvomero

Muonekano wa Jengo la biashara na ofisi la 2D Morogoro 

Mkurugenzi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani akitoa maelezo alipotembela jengo la biashara na ofisi la 2D Morogoro .



    PLOT NO. 31-34 NKOMO, eneo lenye  Magodown  mawili  ambayo hayatumiki kwa sasa kutokana na kuchakaa kwa magodown hayo.

Mkurugenzi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani akiwa ndani ya jengo la godown

PLOT NO 66/2 OLD DSM ROAD

PLOT NO 66/2 OLD DSM ROAD


PLOT NO 53KINGO

Mkuu wa shule ya Sekondari Mzumbe akimkaribisha Dkt. Maulidi Banyani Mkurugenzi Mkuu NHC alipotembelea shuleni hapo.

Moja ya jengo lilikarabatiwa na Shirika la Nyumba la Taifa