Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dkt. Maulidi Banyani alifanya ziara ya siku mbili katika mkoa wa Morogoro na kutembelea miradi mbalimbali akianzia katika Halmashauri ya wilaya ya Malinyi ambapo Shirika la nyumba la Taifa linajenga jengo la Halmashauri ya wilaya ya Malinyi kama Mkandarasi,
Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulidi Banyani ameagiza ifikapo tarehe 29/05/2019 jengo liwe limekamilika na kukabidhiwa kwa Halmashauri.
Baada ya kutoka katika Halmashauri ya wilaya ya Malinyi ziara hiyo ilielekea katika wilaya ya Mvomero ambapo shirika limejenga nyumba 42.
Vilevile Mkurugenzi Mkuu Dkt. Banyani alitembelea Jengo la biashara na ofisi la 2D lililopo Morogoro Mjini, Dkt. Banyani alitoa agizo kwa Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa, Verenanda Seif kuhakikisha wanalitangaza jengo hilo ili lipate wapangaji wa kutosha tofauti na sasa ambapo asilimia 30 tu ndio iliyochukuliwa sehemu kubwa ikiwa ni mabenki
pia akatoa agizo kwa mameneja wote pindi wanapopangisha jengo wawe wanapiga picha jengo kabla ya mpangaji kuingia ili anapoondoka akabidhi likiwa bora kama alivyokabidhiwa na si vinginevyo.
Pia alitembelea Plot No 31- 34 Nkomo, Plot No 66/2 OLD DSM ROAD, PLOT 53 KINGO mwisho alimaza ziara kwa kutembelea Shule ya Sekondari Mzumbe iliyokarabatiwa na Shirika. Mkuu wa Shule alilipongeza Shirika kwa kufanya kazi nzuri na yenye weledi na kutoa wito kwa Serikali kwa miradi kama hiyo wapewe NHC kwani wamefanyakazi nzuri sana na kwa wakati.
Jengo la Halmashauri ya wilaya ya Malinyi linavyoonekana kwa sasa
Dkt. Maulidi Banyani akiwa ameongozana na Kaimu Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa ndani Abdallah Migila pamoja Meneja wa mkoa wa Morogoro Veneranda Seif wakiwa katika mradi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Malinyi.
Mhandisi Hassan Mohamed akitoa maelezo ya mradi kwa Mkurungezi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani
Mhandisi Hassan Mohamed akitoa maelezo ya mradi kwa Mkurungezi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani
Picha ya pamoja kati ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Malinyi na Shirika la Nyumba la Taifa.
Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulidi Banyani akiwa na Kaimu Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa ndani Abdallah Migila, Baraka Killungu wakiwa na Meneja wa mkoa wa Morogoro Veneranda Seif wakiwa katika Nyumba za makazi Mvomero.
Mkurugenzi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani wakijadiliana jambo na Kaimu Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa ndani Abdallah Migila walipotembelea Nyumba za makazi 42 zilizojengwa katika Halmashauri ya wilaya ya Mvomero
Muonekano wa Jengo la biashara na ofisi la 2D Morogoro
PLOT NO. 31-34 NKOMO, eneo lenye Magodown mawili ambayo hayatumiki kwa sasa kutokana na kuchakaa kwa magodown hayo.
Mkurugenzi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani akiwa ndani ya jengo la godown
PLOT NO 66/2 OLD DSM ROAD
PLOT NO 66/2 OLD DSM ROAD
PLOT NO 53KINGO
Mkuu wa shule ya Sekondari Mzumbe akimkaribisha Dkt. Maulidi Banyani Mkurugenzi Mkuu NHC alipotembelea shuleni hapo.
Moja ya jengo lilikarabatiwa na Shirika la Nyumba la Taifa
No comments:
Post a Comment