ON POINT MEDIA

ON POINT MEDIA
Karibuni sana kwa kazi nzuri ya video za harusi mikutano na kadharika

SHIRKA LA NYUMBA LA TAIFA

SHIRKA LA NYUMBA LA TAIFA
NYUMBA YANGU MAISHA YANGU

Monday, 3 December 2018

MKURUGENZI MKUU NHC AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA MOROGORO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dkt. Maulidi Banyani alifanya ziara ya siku mbili katika mkoa wa Morogoro na kutembelea miradi mbalimbali akianzia katika Halmashauri ya wilaya ya Malinyi ambapo Shirika la nyumba la Taifa linajenga jengo la Halmashauri  ya wilaya ya Malinyi kama Mkandarasi,
Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulidi Banyani ameagiza ifikapo  tarehe 29/05/2019 jengo liwe limekamilika na kukabidhiwa kwa Halmashauri.

Baada ya kutoka katika Halmashauri ya wilaya ya Malinyi ziara hiyo ilielekea katika wilaya ya Mvomero ambapo shirika limejenga nyumba  42. 

Vilevile Mkurugenzi Mkuu Dkt. Banyani alitembelea Jengo la biashara na ofisi la 2D lililopo Morogoro Mjini, Dkt. Banyani alitoa agizo kwa Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa, Verenanda Seif kuhakikisha wanalitangaza jengo hilo ili lipate wapangaji wa kutosha tofauti na sasa ambapo asilimia 30 tu ndio iliyochukuliwa sehemu kubwa ikiwa ni mabenki
pia akatoa agizo kwa mameneja wote pindi wanapopangisha jengo wawe wanapiga picha jengo kabla ya mpangaji kuingia ili anapoondoka akabidhi likiwa bora kama alivyokabidhiwa na si vinginevyo.
Pia alitembelea Plot No 31- 34 Nkomo, Plot No 66/2 OLD DSM ROAD, PLOT 53 KINGO  mwisho alimaza ziara kwa kutembelea Shule ya Sekondari Mzumbe iliyokarabatiwa na Shirika. Mkuu wa Shule alilipongeza Shirika kwa kufanya kazi nzuri na yenye weledi na kutoa wito kwa Serikali kwa miradi kama hiyo wapewe NHC kwani wamefanyakazi nzuri sana na kwa wakati.

Jengo la Halmashauri  ya wilaya ya Malinyi linavyoonekana kwa sasa
Dkt. Maulidi Banyani akiwa ameongozana na Kaimu Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa ndani Abdallah Migila pamoja Meneja wa mkoa wa Morogoro Veneranda Seif wakiwa katika mradi wa jengo la Halmashauri  ya wilaya ya Malinyi.


Mhandisi Hassan Mohamed akitoa maelezo ya mradi kwa Mkurungezi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani 



Mhandisi Hassan Mohamed akitoa maelezo ya mradi kwa Mkurungezi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani



Mkurungezi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani akitoa maelekezo wakati alipotembelea mradi huo wa jengo la Halmashauri  ya wilaya ya Malinyi unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa.
Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulidi Banyani akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri  ya wilaya ya Malinyi Mussa Mnyeti  alipotembelea katika mradi wa jengo Halmashauri  ya wilaya ya Malinyi linalojengwa na NHC 


Picha ya pamoja kati ya watumishi wa  Halmashauri  ya wilaya ya Malinyi na Shirika la Nyumba la Taifa.


Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulidi Banyani akiwa  na Kaimu Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa ndani Abdallah Migila, Baraka Killungu  wakiwa na  Meneja wa mkoa wa Morogoro Veneranda Seif wakiwa katika  Nyumba za makazi Mvomero.

Nyumba za makazi 42 zilizojengwa  katika Halmashauri ya wilaya ya Mvomero
Mkurugenzi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani wakijadiliana jambo  na Kaimu Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa ndani Abdallah Migila walipotembelea Nyumba za makazi 42 zilizojengwa  katika Halmashauri ya wilaya ya Mvomero

Muonekano wa Jengo la biashara na ofisi la 2D Morogoro 

Mkurugenzi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani akitoa maelezo alipotembela jengo la biashara na ofisi la 2D Morogoro .



    PLOT NO. 31-34 NKOMO, eneo lenye  Magodown  mawili  ambayo hayatumiki kwa sasa kutokana na kuchakaa kwa magodown hayo.

Mkurugenzi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani akiwa ndani ya jengo la godown

PLOT NO 66/2 OLD DSM ROAD

PLOT NO 66/2 OLD DSM ROAD


PLOT NO 53KINGO

Mkuu wa shule ya Sekondari Mzumbe akimkaribisha Dkt. Maulidi Banyani Mkurugenzi Mkuu NHC alipotembelea shuleni hapo.

Moja ya jengo lilikarabatiwa na Shirika la Nyumba la Taifa 



Wednesday, 28 November 2018

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LACHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI KISARAWE

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akielezea sifa za eneo la Vigungu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani wakati msafara huo wa Mkurugenzi Mkuu ulipokuwa katika eneo la Vigungu kunakotarajiwa kupimwa kwaajili ya uendelezaji wa makazi na shughuli mchanganyiko. Eneo hilo liko katika Barabara kuu iendayo Kibaha na eneo limetenganishwa na viwanda kwa barabara hiyo iendayo Kibaha. Matangi mawili ya kuhifadhia maji, yenye uwezo wa lita milioni tano, yatajengwa katika maeneo ya karibu na hapo, kwa ajili ya viwanda na makazi mapya; na Minarani kwa ajili ya mji wa Kisarawe kwa gharama ya Sh bilioni 10.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani akitia saini kwenye kitabu cha wageni cha Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe alipotembelea ofisi hizo kabla ya kutembelea baadhi ya fursa za uwekezaji  wilayani Kisarawe ambapo Shirika la Nyumba la Taifa linaweza kushirikiana na Wilaya hiyo katika uwekezaji maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na eneo la  Community Hall,  Stendi ya zamani na eneo kunakotarajiwa kuanza kupimwa viwanja vya makazi na shughuli mchanganyiko la Vigungu lililopo nje kidogo ya mji wa Kisarawe. 
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza na ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa, ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk. Maulidi Banyani. 
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtela Mwampamba akiukaribisha ujumbe kutoka NHC na kisha kuwatambulisha maafisa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. 
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk. Maulidi Banyani akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kuelekea eneo la  Community Hall lililopo jirani kabisa na zilipo Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk. Maulidi Banyani akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo walipotembelea eneo la Stendi ya zamani Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani leo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk. Maulidi Banyani akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo walipotembelea eneo la Stendi ya zamani Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani leo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtela Mwampamba akielekeza jambo msafara huo ulipokuwa katika eneo la Vigungu kunakotarajiwa kupimwa kwaajili ya uendelezaji wa makazi na shughuli mchanganyiko eneo hilo liko katika Barabara kuu iendayo Kibaha na eneo limetenganishwa na viwanda kwa barabara hiyo iendayo Kibaha. Matangi mawili ya kuhifadhia maji, yenye uwezo wa lita milioni tano, yatajengwa katika maeneo ya hayo, kwa ajili ya viwandana makazi mapya; na Minarani kwa ajili ya mji wa Kisarawe kwa gharama ya Sh bilioni 10.

Eneo la  Vigungu kunakotarajiwa kupimwa kwaajili ya uendelezaji wa makazi na shughuli mchanganyiko eneo hilo liko katika Barabara kuu iendayo Kibaha na eneo limetenganishwa na viwanda kwa barabara hiyo iendayo Kibaha. Matangi mawili ya kuhifadhia maji, yenye uwezo wa lita milioni tano, yatajengwa katika maeneo yaVigungu, kwa ajili ya viwandana makazi mapya; na Minaranikwa ajili ya mji wa Kisarawe kwagharama ya Sh bilioni 10.
Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani na ujumbe wake akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kwenye eneo la Vigungu wakati msafara huo wa Mkurugenzi Mkuu ulipokuwa katika eneo la Vigungu kunakotarajiwa kupimwa kwaajili ya uendelezaji wa makazi na shughuli mchanganyiko.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani na ujumbe wake akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kwenye eneo la Vigungu wakati msafara huo wa Mkurugenzi Mkuu ulipokuwa katika eneo la Vigungu kunakotarajiwa kupimwa kwaajili ya uendelezaji wa makazi na shughuli mchanganyiko.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza na ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa, ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk. Maulidi Banyani. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani na ujumbe wake akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo mbele ya ofisi  ya Mkuu wa Wilaya.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo mbele ya ofisi  ya Mkuu wa Wilaya.

Kaimu Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.
Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.

Monday, 26 November 2018

NHC YASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI YA KILOMITA TANO

Matembezi ya Hisani ya kilomita tano (5) ya Kusanyiko la Waliowahi kuhitimu na wanaokitakia mema Chuo Kikuu cha Ardhi yalifanyika tarehe 24/11/2018 (Jumamosi)  matembezi yalianza saa kumi na mbili asubuhi kwenye jengo la utawala la Chuo Kikuu Ardhi hadi Container na Dispensary Chuo kikuu DSM na kurudi ARU Washiriki kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) walishiriki kikamilifu  wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulidi Banyani. mara baada ya matembezi hayo kulifanyika mazoezi ya viongo pamoja na michezo mbalimbali. Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulidi Banyani akatoa agizo kwa kitengo cha Utawara waandae mkakati utakao pelekea kila wiki ya mwisho wa mwezi kuwe utaratibu wa kufanaya  mazoezi na matembezi ya namna hii  na  yatakuwa ni lazima kila mwezi mara moja na itaitishwa roll call ili kuhakikisha ushiriki na kuimarisha afya za wafanyakazi.
Mazoezi ni Afya, furaha na hujenga pia umoja.
Wadau mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa NHC wakiwa katika Matembezi ya hisani ya kilomita tano ya kusanyiko la waliowahi kuhitimu Chuo Kikuu Ardhi.

Wadau mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa NHC wakiwa katika Matembezi ya hisani ya kilomita tano ya kusanyiko la waliowahi kuhitimu Chuo Kikuu Ardhi.

Wadau mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa NHC wakiwa katika Matembezi ya hisani ya kilomita tano ya kusanyiko la waliowahi kuhitimu Chuo Kikuu Ardhi.

Wadau mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa NHC wakiwa katika Matembezi ya hisani ya kilomita tano ya kusanyiko la waliowahi kuhitimu Chuo Kikuu Ardhi

Wadau mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa NHC wakiwa katika Matembezi ya hisani ya kilomita tano ya kusanyiko la waliowahi kuhitimu Chuo Kikuu Ardhi

Wadau mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa NHC wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya matembezi ya hisani ya kilomita tano ya kusanyiko la waliowahi kuhitimu Chuo Kikuu Ardhi.

Wadau mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa NHC wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya matembezi ya hisani ya kilomita tano ya kusanyiko la waliowahi kuhitimu Chuo Kikuu Ardhi.
Wadau mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa NHC wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya matembezi ya hisani ya kilomita tano ya kusanyiko la waliowahi kuhitimu Chuo Kikuu Ardhi


Wadau mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa NHC wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya matembezi ya hisani ya kilomita tano ya kusanyiko la waliowahi kuhitimu Chuo Kikuu Ardhi.




Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka katikati Mwenyekiti wa Bodi Dkt Sophia Kongela, Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulidi Banyani, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NHC walioshiriki katika matembezi ya hisani ya kilomita tano ya kusanyiko la waliowahi kuhitimu Chuo Kikuu Ardhi.





Mkurugenzi Mkuu NHC Dkt. Maulidi Banyani pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NHC wakiwa katika picha ya pamoja na aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu NHC Ndg. Haruna Masebu


Shindano la kuvuta kamba kati ya NHC na wadau wa Chuo kikuu Ardhi katika shindano Chuo kikuu Ardhi walishinda.

Shindano la Mbio mita 100 umri kuazia 40 - 60 ambapo Ndgu Sam Metili wa NHC alishinda akifatiwa na Albinus Simba 
Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulidi Banyani pia alishiliki mbio hizo
upande wa kinadada mbio mita 100 alishinda  Allana Ngonyani akifatiwa na Mwasiti Jimmy wote kutoka NHC

                     Shindano la kula Apple 






Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulidi Banyani akipokea Kombe la Mshiriki bora wa matembezi ya hisani ya kilomita tano ya kusanyiko la waliowahi kuhitimu Chuo Kikuu Ardhi.



Kikosi cha Ushindi