ON POINT MEDIA

ON POINT MEDIA
Karibuni sana kwa kazi nzuri ya video za harusi mikutano na kadharika

SHIRKA LA NYUMBA LA TAIFA

SHIRKA LA NYUMBA LA TAIFA
NYUMBA YANGU MAISHA YANGU

Sunday, 28 October 2018

WAZIRI LUKUVI ALITAKA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA NHC KUWA MFANO KATIKA KUSIMAMIA NYUMBA ZAKE



 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi,  akiwa na Meneja wa Mkoa Juma Kiaramba alipowasili katika ofisi za shirika la Nyumba  la Taifa Mkoa wa Kilimanjaro

  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi,akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la nyumba la Taifa mkoa wa kilimanjaro

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za shirka la nyumba mkoa wa kilimanjaro

 Meneja wa shirika la nyumba mkoa wa Kilimanjaro Juma Kiaramba akisoma taarifa ya mkoa kwa w  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi

 wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Kilimanjaro
 Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Kilimanjaro akisoma taarifa ya mkoa

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, akiongea na wafanyakazi wa Shirika la nyumba la Taifa mkoa wa Kilimanjaro
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi,akitoka katika ofisi za Shirika la Nyumba la Tiafa mara baada ya kufanya ziara


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. William Lukuvi amelitaka shirika la nyumba la Taifa (NHC) liwe mfano katika ujenzi, kuhifadhi na kutunza nyumba zake pamoja na kujenga nyumba za gharama nafuu kwa wananchi.

Mhe Lukuvi  alisema hayo alipotembelea ofisi za shirika hilo katika mkoa wa Kilimanjaro akiwa katika ziara ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika wilaya za Hai, Moshi na Same.

Alisema NHC lazima iwe mfano kwa taasisi nyingine katika ujenzi  wa nyumba bora na kuwapangisha wapangaji  kwa kipindi cha mwezi mmoja mmoja badala ya utaratibu uliozoeleka wa kupangisha watu kwa kipindi cha miezi sita au mwaka mmoja sambamba na kuepuka vishoka katika upangishaji nyumba zake.

Aidha, amelitaka shirika la NHC kuwa na mkakati maalum wa kukarabati nyumba zake na kubainisha kuwa haiwezekani shirika kubwa kama hilo kuwa na nyumba nyingi katika vitovu vya miji lakini zikiwa  zimechoka na kusisitiza kuwa asingependa kusikia shirika hilo linakuwa na nyumba mbovu.

Amelitaka shirika la nyumba la taifa kujipanga vizuri na kuhakikisha linashirikiana na halmashauri  zote nchini  kujenga nyumba kwa ajili ya watumishi  pamoja na kujitangaza katika shughuli zake kwa kuwa  lina kampuni imara ya ujenzi yenye wataalanu na inayoweza kujenga majengo mbalimbali kama vile  shule,hospitali, vituo vya afya, vituo vya afya, vyuo na majengo ya watu binafsi.

Lukuvi amelitaka shirika kuimarisha kitengo cha huduma kwa wateja na kutembelea wateja kwa lengo la kujua matatizo ya wapangaji katika nyumba zao ili kutatua kero zao.

Kwa upande wake Meneja wa NHC mkoa wa Kilimanjaro Bw......alimueleza Lukuvi kuwa Shirika lake limekuwa na ushirikiano na halmashauri katika mkoa huo na tayari wameshaanza majadiliano kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika halmashauri ya Manispaa ya Moshi kujenga jumla ya nyumba ishirini na tano.

No comments:

Post a Comment