SHIRIKA LA NYUMBA LAIKABIDHI BENKI KUU MAJENGO KWA AJILI YA WAFANYAKAZI
WAKE MTWARA
Benki Kuu ya Tanzania imekabidhiwa jengo la ghorofa tano lililojengwa na
NHC eneo la Shangani Mtwara, lenye
nyumba kumi ilizonunua kwa ajili ya Wafanyakazi wake wanaotarajiwa kuhamia
Mtwara mwezi Septemba mwaka huu ikiwa ni ishara ya Benki hiyo kuanza kutoa
huduma katika kanda ya kusini mwa Tanzania. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
Prefesa Benno Ndulu amelishukuru Shirika la Nyumba kwa kuwajengea nyumba bora
za kisasa. Aidha, Benki Kuu ya Tanzania imenunua nyumba 40 zinazojengwa na NHC
eneo la Rahaleo Mtwara ambazo zinatarajiwa kukabidhiwa mwezi Septemba mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akimkaribisha Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prefesa Benno Ndulu alipowasili eneo la shangani kukabidhiwa Nyumba walizonunua.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu aliongea na hadhira wakati wa sherehe ya kuikabidhi Benki Kuu ya Tanzania Nyumba walizonunua kwa ajili ya wafanyakazi wa banki hiyo.
Viongozi wandamizi kutoka Banki kuu ya Tanzania
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prefesa Benno Ndulu akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Shirika la Nyumba kwa kuwajengea nyumba bora za kisasa.
Gavana wa Benki Kuu na Mkurugenzi Mkuu wa NHC wakisaini hati ya kukabidhiana nyumba zilizonunuliwa na Banki Kuu eneo la Shangani Mtwara.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akimkabidhi Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prefesa Benno Ndulu Cheti cha ubora wa Jengo kuashiria kuwa jengo lao walilonunua NHC ni salama kukaliwa na wafanyakazi wa Banki hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akimkabidhi Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prefesa Benno Ndulu mfano wa ufunguo wakati alipo mkabidhi nyumba walizo nunua kwa ajili ya watumishi wa Banki Kuu tawi la Mtwara.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prefesa Benno Ndulu akikata utepe kuashilia kukabidhiwa Nyumba walizonunua kwa ajili ya wafanyakazi wa Banki Kuu tawi la Mtwara.
Picha ya pamoja ya Viongozi wa NHC na BOT baada ya kukabidhiana nyumba za makazi zilizojengwa na NHC eneo la Shanghai Mtwara
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akimuonyesha Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prefesa Benno Ndulu Mazingira ya nyumba hizo.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Ndg. Julian Banzi Raphael na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu wakifurahia jambo walipotembelea mradi wa Rahaleo Mtwara, Ambapo Benki Kuu ya Tanzania imenunua nyumba za makazi 40 kwa ajili ya watumishi wa Banki Kuu tawi la Mtwara.
Mkrugenzi wa Ujenzi Mhandisi Haikamen Mlekio akimuhakikishaia Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prefesa Benno Ndulu kuwa nyumba 40 zilizobaki zitakamilika kwa wakati waliokubaliana
No comments:
Post a Comment